Forum where rangeland experts, trainees and stakeholders meet to discuss and exchange social and scientific ideas for livestock production and range ecosystem sustainability.
Monday, 27 February 2017
SIKU YA NYANDA ZA MALISHO TANZANIA
SIKU YA NYANDA ZA MALISHO TANZANIA.
Ni historia nyingine tumeiweka katika nchi yetu kutoa taswira na kujadiliana kuhusu hali ya nyanda za malisho hapa nchini ambalo ndilo jambo kubwa kwa wafugaji.
Aidha kwa niaba ya wana-TRSA nitoe shukrani zangu za dhati kwa walimu wetu (RST) ambao wamekuwa chachu kubwa ya mafanikio makubwa tuliyoyaona leo, viongozi wetu wa RST ambao sio walimu wetu, wageni waliokuwepo, waandishi wa habari, wana-TRSA wote (RST wa baadae) na kila mmoja aliyefanikisha hili jambo. Hakika jamii inatuitaji tukaitumikie. Sisi kama wana-TRSA ni muda muafaka wa kuzidi kujituma zaidi na kubuni zaidi njia za kuisaidia jamii zetu haswa hizi za wafugaji.
By Makamu m/kiti TRSA.
Saturday, 25 February 2017
MCHANGO WA WILAYA YA KILINDI MKOANI TANGA KWA WAFUGAJI.
Hii ni sehemu inayopatikana wilayani Kilindi mkoani Tanga.Ni kati ya sababu kubwa zinazowafanya wafugaji kutoka sehemu mbalimbali kusafiri na mifugo kuelekea wilayani Kilindi, wafugaji husafiri kutoka sehemu mbalimbali kama wilaya za Simanjiro na Kiteto kuja eneo hili kulambisha mifugo yao udongo wenye madini ya chumvi chumvi ili kupata joto.
Hata maji yake pia yana kiasi kingi cha madini ya chumvi chumvi ambapo wakati mwingine, mifugo hunywa haya maji na kufikia kiwango kinachohitajika mwilini cha madini haya ya chumvi chumvi.
Je, serikali ina mpango wowote wa kulilinda na kulitunza hili eneo?
Kinachosikitisha ni jinsi shughuli za kilimo zinavyoathiri hili eneo...hakika nguvu kubwa inahitajika.
MATATIZO YASABABISHWAYO NA UVAMIZI WA VICHAKA NDANI YA NYANDA ZA MALISHO.
Uvamizi wa vichaka ndani ya nyanda za malisho umekuwa ni tatizo kubwa sana hapa nchini katika maeneo yetu ya machunga.
Ikizingatiwa ufugaji wa wafugaji wengi wa kitanzania ni ufugaji huria (free ranging).
Maeneo mengi yamepoteza ubora wake katika kuhudumia mifugo inayotegemea rasilimali zake na kusababisha uhamaji wa wafugaji kutafuta maeneo mengine yaliyo salama zaidi.
Zifuatazo ni athari za vichaka ndani ya machunga.
1. Kuongeza ushindani ardhini dhidi ya malisho mengine kwenye upande wa madini, maji, mwanga n.k
2. Kuzuia ukuaji wa malisho sababu vichaka huathiri ukuaji wa malisho haswa katika upatikanaji wa mwanga wa jua.
3. Kuzuia uwezo wa mifugo kufikia malisho hasa grazers.
4. Kuwa kivutio cha wadudu wasababishao magonjwa kwa mifugo, mfano mbungo.
5. .......................
SIKU YA NYANDA ZA MALISHO KITAIFA 27/02/2017- GLONENCY 88 HOTEL.
Hii ni siku muhimu sana kwa taifa letu na jamii nzima(wafugaji na wasio wafugaji).
Hatuwezi kukataa faida za ufugaji katika kuangalia faida zitokanazo na mifugo pamoja na mazao ya mifugo husika katika jamii zetu. Ni kweli hakuna shughuli yoyote ile ya kibinadamu yenye faida pekee pasipo kuwa na madhara yake.
Aidha, siku hii muhimu inayokutanisha wadau wote wanaohusika ama kuwa na muingiliano na nyanda za malisho wanapokutana sehemu moja na kujadili changamoto mbalimbali kuhusu ufugaji pamoja na nyanda za malisho hapa nchini.
Aidha, shukrani za dhati ziende katika uongozi mzima wa RANGELAND SOCIETY OF TANZANIA pamoja Prof. E. J Mtengeti kwa jitihada zao za kulitumikia taifa katika kutoa ujuzi wao kuisaidia jamii pamoja na kutupa nafasi wanafunzi wa taaluma hii kujifunza mambo mengi zaidi.
Ni wakati muafaka sasa sisi kama wanafunzi kuonesha nguvu zetu katika kusapoti jitihada hizi zinazofanywa na wahadhiri wetu.
Kuanzia mwaka wa kwanza hadi wa tatu kushiriki katika mkutano huu wa kitaifa. Kuzitambua mada husika na kuchangia mawazo yetu juu ya mada ambazo zitaenda kusomwa na wanafunzi wenzetu siku hiyo.
Tunaamini katika umoja wetu tutaijenga TRSA na RST.
TRSA ya sasa ndiyo RST ya baadae.
Makamu mwenyekiti- TRSA.
Subscribe to:
Posts (Atom)