Saturday, 25 February 2017

SIKU YA NYANDA ZA MALISHO KITAIFA 27/02/2017- GLONENCY 88 HOTEL.

Hii ni siku muhimu sana kwa taifa letu na jamii nzima(wafugaji na wasio wafugaji). Hatuwezi kukataa faida za ufugaji katika kuangalia faida zitokanazo na mifugo pamoja na mazao ya mifugo husika katika jamii zetu. Ni kweli hakuna shughuli yoyote ile ya kibinadamu yenye faida pekee pasipo kuwa na madhara yake. Aidha, siku hii muhimu inayokutanisha wadau wote wanaohusika ama kuwa na muingiliano na nyanda za malisho wanapokutana sehemu moja na kujadili changamoto mbalimbali kuhusu ufugaji pamoja na nyanda za malisho hapa nchini. Aidha, shukrani za dhati ziende katika uongozi mzima wa RANGELAND SOCIETY OF TANZANIA pamoja Prof. E. J Mtengeti kwa jitihada zao za kulitumikia taifa katika kutoa ujuzi wao kuisaidia jamii pamoja na kutupa nafasi wanafunzi wa taaluma hii kujifunza mambo mengi zaidi. Ni wakati muafaka sasa sisi kama wanafunzi kuonesha nguvu zetu katika kusapoti jitihada hizi zinazofanywa na wahadhiri wetu. Kuanzia mwaka wa kwanza hadi wa tatu kushiriki katika mkutano huu wa kitaifa. Kuzitambua mada husika na kuchangia mawazo yetu juu ya mada ambazo zitaenda kusomwa na wanafunzi wenzetu siku hiyo. Tunaamini katika umoja wetu tutaijenga TRSA na RST. TRSA ya sasa ndiyo RST ya baadae. Makamu mwenyekiti- TRSA.

No comments:

Post a Comment