Sunday, 28 May 2017

THE GREAT 2014-2017 RANGE CLASS.

 BAADHI YA PICHA ZA MATUKIO YALIYOPATA KUTUUNGANISHA KWA KIPINDI CHETU HATA SASA TUNAPOELEKEA KUMALIZA SAFARI YETU.
Katika kipindi chote tulichoishi pamoja katika mazingira ya chuo, tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu na hatimaye sasa safari tunaelekea kuimaliza. Leo ntatoa baadhi ya picha mbalimbali za matukio yaliyokuwa ya furaha tangu tukiwa mwaka wa kwanza na hata sasa tunapokaribia kuhitimu masomo yetu. Twende pamoja katika kumbukumbu hizi....

 
The dream team mwaka wa kwanza hapo
Siku tuliyokaribishwa SUA       





pasture establishment-yr 2
Maandalizi ya saileji- yr2
FPT- Stendi mpwapwa




Maandalizi ya kupanda C. ciliaris-yr2



 




FPT mpwapwa- Animal grazing beahior yr2
FPT mpwapwa- baada ya kujifunza fire mgt

Long trip to KITETO DC
FPT- bwawani Namelock                











FPT- Tukiwa na wafugaji
FPT- Tukiwa kata ya makame Kiteto dc (Maasai mara)














FPT-Kisima cha maji                 

FPT-Tukiwa na Dr. Sangeda Kiteto










FPT- KITETO DC Tukipata mapitio ya mafunzo yetu.
FPT-Chanzo cha chumvi kwa mifugo Kilindi dc

FPT- Trip to Kilindi dc










FPT-Prof Mahonge akitoa neno Kilindi dc
FPT- Kwamaligwa dam Kilindi dc

FPT- Kilindi dc

Picha ya pamoja na wafugaji












FPT- Kikao na wafugaji kijiji cha Elerai
FPT-Kikao na wafugaji kijiji cha Elerai










Range day 2017
Range day 2016










Range improvement
FPT- Biodervesity









HAKIKA HII NI THE DREAM TEAM 2014-2017









Tunajivunia umoja wetu katika shughuli mbalimbali kwa takribani miaka mitatu tuliyodumu pamoja. Aidha, shukrani kwa walimu wetu kwa kila mmoja alivojitoa kuhakikisha tunafikia lengo lililokusudiwa.

KUMBUKUMBU HII IMEANDALIWA NA
Linus, Floidin John

                                 
















Sunday, 14 May 2017

MIMEA INAYOWEZA KUTUPA VIASHIRIO VYA HALI YA MACHUNGA.

Chanzo ni Prof E.J. MTENGETI  
Idara ya sayansi ya mifugo,samaki na malisho
Sokoine University of agriculture.
       
 Ili kutambua hali ya machunga lazima kutambua mimea muhimu yenye kuashiria hali ya machunga. Uwepo au kutokuwepo kwa mimea fulani ndani ya machunga ni kiashiria tosha cha hali ya machunga. Na hii itakupa fursa kutambua kama unatakiwa kuchukua hatua gani madhubutu kurekebisha au kudumisha hali hiyo. Mimea iliyotolewa maelezo (siyo picha) na Prof. E.J. Mtengeti ni kama ifuatavyo:-

Kutambua afya ya machunga
Brachiaria brizantha
 a) Kuna mimea ambayo ukigundua  inapungua sana ndani ya machunga (decreasers) basi ujue malisho yanachungiwa sana. Mimea inayopendelewa sana na mifugo ndiyo hupungua kadri machunga yanavyochungiwa kwa mudamrefu zaidi. mfano mzuri ni Brachiaria brizantha.





Sporobolus pyramidalis.
b)Kuna mimea ambayo huongezeka kadri machunga yanavyozidi kuchungiwa (increasers). Mimea hii siyo yenye kupendelewa na mifugo. Manake ni kwamba mimea inayopendelewa (decreasers) hupungua na mimea mingine(increasers) huibuka. Ukigundua mimea hiyo basi ni kiashiria cha kuzidisha kuchunga katika eneo hilo. Mfano ni Sporobolus pyramidalis.

Mimea hii ni hatari sana, kwa sababu ukiiruhusu iendelee kukua huweza kuathiri mimea mingine ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya mifugo. Hivyo mimea ya aina hii inatakiwa kudhibitiwa haraka sana mara tu baada ya kuona viashiria vyake.
c) Mimea vamizi (invaders). Mimea yenye sifa za kipengele (a) na (b) inapochungiwa sana na kuliwa
Dactyloctenium aegyptium
Rhynchelytrum repens
basi hupungua ndani ya machunga kisha mimea mipya isiyoliwa
kabisa na mifugo huvamia eneo hilo. Mimea hiyo ni kama vile Dactyloctenium aegyptium na Rhynchelytrum repens. Mimea hii haitakiwi kabisa ndani ya machunga kwa sababu ya madhara yake kama vile, kupunguza chakula cha mifugo, kushambulia mimea muhimu pamoja na uwezo wake mdogo wa kulinda udongo dhidi ya tatizo la mmomonyoko.

Mimea inayoweza kuashiria uwepo wa maji.
Acacia xanthophlea
Sycamore
Kuna mimea ndani ya machunga ambayo ni kiashiria kizuri cha uwepo wa maji karibu kabisa na uso wa dunia. Mimea hii ni muhimu haswa kwa meneja/ mfugaji anayetaka kuchimba kisima kwa ajili ya kupata maji ya mifugo na kumwagilizia malisho yake. Mimea hii ni kama vile, Sycamore, Acacia xanthophlea, Acacia elatior.


Kutambua hali ya udongo.
Kuna mimea ndani ya machunga ambayo hutoa viashiria vya hali ya udongokatika eneo husika. Mfano ni,
Cynodon nlemfuensis
1) Cynodon nlemfuensis hii mimea huashiria uwepo wa wingi nitrojeni katika udongo wa eneo husika na udongo wenye unyevunyevu wa kutosha.

Conyza stricta
2) Conyza stricta  hii mimea pia hupendelea udongo wenye nitrojeni nyingi.
Hivyo ni kiashiria cha nitrojeni nyingi kwenye machunga.
3. Imperata cylindrica huashiria udongo wenye pH ndogo yaani asili ya asidi.




Imperata cylindrica

IMEANDALIWA NA MAKAMU MWENYEKITI TRSA
Linus, Floidin John

Saturday, 13 May 2017

MALISHO YENYE KUWEZA KUSTAHIMILI HALI YA UKAME.

NYASI ZENYE UWEZO WA KUSTAHIMILI MAENEO YENYE ASILI YA  UKAME
  1. Cenchrus ciliaris  (Buffel grass)
Buffel grass
Ni nyasi zinazolimwa sana kwa ajili ya kuzalisha
chakula cha mifugo. Zina uwezo wa kustahimili ukame kwa muda mrefu hivyo kupendekezwa kama nyasi zenye kuweza kulimwa maeneo kame hapa nchini kama Dodoma, Tabora na Singida. Hutoa mizizi yenye kwenda ardhini umbali wa hadi meta 2, hivyo huweza kufyonza maji ardhini mbali zaidi. Ni rahisi kupanda na hutoa malisho kwa wingi haswa zikipandwa na mbolea. Ikivunwa mwanzoni kabisa baada ya kuchomoza maua,huzalisha malisho mengi na bora ambayo huweza kutunzwa kama hei (hay). Akiba hii huweza kutumika wakati wa kiangazi kulishia mifugo. Buffel grass hustahimili moto (FAO, 2010). Haina uwezo wa kustahimili maeneo yenye kukumbwa na mafuriko (waterlogging area) na huweza kufa kwa baada ya takribani siku  6 (Ecoport, 2010). Huweza kuvumilia kuchungiwa (over grazing) hata kukanyagwa( trampling.

2. Urochloa mosambicensis
Sabi grass
Lugha za kawaida hujulikana kama Sabi grass (Australia), gonya grass (Zimbabwe) n.k.

Hizi ni nyasi zenye kustahimili ukame na kudumu zaidi ya mwaka mmoja (perennial). Hutofautiana kimo au wastani wa ukuaji pamoja na tabia (habit) ya ukuaji kutokana na sababu mbali mbali kama hali ya hewa ya eneo husika(climate), udongo (edaphic factors) n.k
Huota katika udongo tofauti ijapokuwa huitaji zaidi udongo wenye mbolea, kuanzia udongo wenye asili ya ufinyazi (clay soil) na ule wenye asili ya kichanga (sandy soil). Huweza kustahimili udongo  wenye asili ya u-asidi, alkali na chumvi chumvi.

Hata hivyo, kwa nchini mwetu wafugaji wetu hawajajikita katika ulimaji wa nyasi aina hii lakini ni chanzo kizuri cha chakula kwa ajili ya mifugo.
Ni nyasi ambayo haijathibitika kuwa na sumu yoyote kwa mifugo au kuwa na uhusiano na magonjwa, hivyo ni chakula kisicho na madhara kwa mifugo


3. Eragrostis superba (Masai love grass)
Masai love grass
Hujiotea kwa asili hapa nchini sababu ya wakulima au wafugaji wengi kutokujikita katika kilimo cha nyasi za kulishia mifugo.
 Hukua kwa haraka sana na huwa na hali ya umbijani kwa takribani mwaka mzima. Huweza kustahimili sehemu zenye udongo wa chumvi chumvi na alkali. Hustawi zaidi katika maeneo yenye udongo asili ya kichanga ijapokuwa hata udongo mwingine kama mfinyanzi hustawi. Hata hivyo ijapokuwa hukua haraka lakini hupoteza ubora(stemmy and unpalatable) kwa ajili ya mifugo kadri inavyozidi kukomaa pia kiwango cha virutubisho hushuka sana.



4. Bothriochloa insculpta ( Creeping bluegrass)
Creeping bluegrass

Hutumika kama nyasi za kuchungia au kutengenezea hei(hay)
 katika mashamba ya kufuga ng'ombe wa nyama (hukataliwa na ng'ombe wa maziwa).

Huweza kutumika kwa kuchungia au kukata nyasi na kulishia bandani (cut and carry). 

Ni bora zaidi kama hazijakomaa sana sababu ubora wake(palatability) hupungua kadri nyasi zinavyokomaa.

 Hustahimili ukame, kuchungiwa(heavy grazing) moto na 
mafuriko japo ni kwa kipindi kifupi tu. 
Huweza kustawi katika aina tofauti ya udongo japo haistawi vizuri maeneo yenye udongo wa kichanga . 
 Nyasi hizi hazistawi katika maeneo yenye kivuli au udongo wa asidi.


 MALISHO AINA YA MIKUNDE YENYE UWEZO WA KUSTAHIMILI MAENEO YENYE ASILI YA  UKAME


 1. Stylosanthes humilis


 Uwezo wake wa kutengeneza nitrojeni (nitrogen fixtion), kustahimili ukame, kuboresha hali ya udongo na kuwa chanzo cha protini kwa mifugo ni kati ya faida za huu mkunde. Mkunde huu una uwezo wa kutumia(extract) hata madini ya fosiforasi yaliyo  kidogo sana kutumika kwa ajili ya mimea mingine. Huweza kuoteshwa kwa kuchanganywa na baadhi ya nyasi zisizo zalisha kivuli kama vile Cenchrus ciliaris, Heteropogon contortus na Urochloa mosambicensis. Mkulima anaweza kuchungia moja kwa moja, kukata na kulishia bandani, kutengeneza hei au saileji. Hustahimili ukame pamoja na udongo wa kichanga au tifutifu. Hata hivyo, imethibitika mikunde hii kuwa sumu kwa baadhi ya kupe wasababishao magonjwa kwa ng'ombe (acaricidal effects) (Muro Castrejón et al., 2003; Fernandez-Ruvalcaba et al., 1999).

2. Stylosanthes hamata

Huu mkunde hauna utofauti na mkunde uliotangulia hapo juu katika ustahimilivu na matumizi yake kwa ajili ya mifugo.








Hayo ni baadhi ya malisho yawezayo kustahimili ukame na kuwa msaada kwa mfugaji.....



IMEANDALIWA NA MAKAMU MWENYEKITI- TRSA
Linus, Floidin John.  

Tuesday, 2 May 2017

Monday, 1 May 2017

Kwa ufupi kuhusu Sabi grass.

Kisayansi hujulikana kama Urochloa mosambicensis na kwa lugha za kawaida hujulikana kama Sabi grass (Australia), gonya grass (Zimbabwe) n.k.

Hizi ni nyasi zenye kustahimili ukame na kudumu zaidi ya mwaka mmoja (perennial). Hutofautiana kimo au wastani wa ukuaji pamoja na tabia (habit) ya ukuaji kutokana na sababu mbali mbali kama hali ya hewa ya eneo husika(climate), udongo (edaphic factors) n.k
Huota katika udongo tofauti ijapokuwa huitaji zaidi udongo wenye mbolea, kuanzia udongo wenye asili ya ufinyazi (clay soil) na ule wenye asili ya kichanga (sandy soil). Huweza kustahimili udongo  wenye asili ya u-asidi, alkali na chumvi chumvi.

Hata hivyo, kwa nchini mwetu wafugaji wetu hawajajikita katika ulimaji wa nyasi aina hii lakini ni chanzo kizuri cha chakula kwa ajili ya mifugo.
Ni nyasi ambayo haijathibitika kuwa na sumu yoyote kwa mifugo au kuwa na uhusiano na magonjwa, hivyo ni chakula kisicho na madhara kwa mifugo.
Katika maeneo mengi hapa nchini aina hii ya nyasi hupatikana kwa kujiotea kwa asili. Mfugaji anaweza kuvuna na kuitunza nyasi hii kwa mfumo wa hei (hay) au saileji(silage).
Nyasi hizi hupendwa na mifugo zikiwa katika hali ya ubichi lakini pia zinapokuwa kavu(hay) bado mifugo huweza kula bila tatizo lolote.

Kwa mfugaji mwenye eneo lenye nyasi hizi anaweza kulitenga na kulitunza kwa ajili ya kuvuna nyasi na kuzitunza hadi msimu wa kiangazi. Labda tu, nyasi hizi hazina uwezo wa kustahimili mafuriko. Nyasi hizi hustahimili kuchungiwa lakini pia huweza kustahimili moto.


Imeandaliwa na makamu mwenyekiti-TRSA
Linus, Floidin John