Monday, 1 May 2017

Kwa ufupi kuhusu Sabi grass.

Kisayansi hujulikana kama Urochloa mosambicensis na kwa lugha za kawaida hujulikana kama Sabi grass (Australia), gonya grass (Zimbabwe) n.k.

Hizi ni nyasi zenye kustahimili ukame na kudumu zaidi ya mwaka mmoja (perennial). Hutofautiana kimo au wastani wa ukuaji pamoja na tabia (habit) ya ukuaji kutokana na sababu mbali mbali kama hali ya hewa ya eneo husika(climate), udongo (edaphic factors) n.k
Huota katika udongo tofauti ijapokuwa huitaji zaidi udongo wenye mbolea, kuanzia udongo wenye asili ya ufinyazi (clay soil) na ule wenye asili ya kichanga (sandy soil). Huweza kustahimili udongo  wenye asili ya u-asidi, alkali na chumvi chumvi.

Hata hivyo, kwa nchini mwetu wafugaji wetu hawajajikita katika ulimaji wa nyasi aina hii lakini ni chanzo kizuri cha chakula kwa ajili ya mifugo.
Ni nyasi ambayo haijathibitika kuwa na sumu yoyote kwa mifugo au kuwa na uhusiano na magonjwa, hivyo ni chakula kisicho na madhara kwa mifugo.
Katika maeneo mengi hapa nchini aina hii ya nyasi hupatikana kwa kujiotea kwa asili. Mfugaji anaweza kuvuna na kuitunza nyasi hii kwa mfumo wa hei (hay) au saileji(silage).
Nyasi hizi hupendwa na mifugo zikiwa katika hali ya ubichi lakini pia zinapokuwa kavu(hay) bado mifugo huweza kula bila tatizo lolote.

Kwa mfugaji mwenye eneo lenye nyasi hizi anaweza kulitenga na kulitunza kwa ajili ya kuvuna nyasi na kuzitunza hadi msimu wa kiangazi. Labda tu, nyasi hizi hazina uwezo wa kustahimili mafuriko. Nyasi hizi hustahimili kuchungiwa lakini pia huweza kustahimili moto.


Imeandaliwa na makamu mwenyekiti-TRSA
Linus, Floidin John

No comments:

Post a Comment