Sisi kama chama cha wanafunzi tunaosomea usimamizi na uendelezaji wa nyanda za malisho (TRSA), tunayo masikitiko makubwa sana juu ya kifo cha mzee wetu pia mwalimu wetu Mr. Protace.
Aidha taarifa hizi zimetushtua sana maana mara ya mwisho ni tulipomuona katika maonesho ya kumbukumbu ya waziri mkuu wa zamani wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, marehemu Mh. Edward Moringe Sokoine pale katika viwanja vya Chuo cha Kilimo cha Sokoine (Mazimbu campus).
Tunatoa pole kwa wanafamilia wote waliokutwa na msiba huu, idara ya sayansi ya wanyama, malisho na samaki (SUA), viongozi wa Chama cha Wadau wa Nyanda za malisho Tanzania (RST) na wadau wote walionufaika na ujuzi wa mzee wetu.
TRSA tunamuombea kwa mwenyezi Mungu amrehemu mzee wetu.
Tangulia mzee wetu hakika uliyoyafanya ni mengi sana na ni makubwa mno. Daima ulijaribu kutujenga katika misingi ya kupenda kila tulichokuwa tukikifanya. Ulitamani kila ulichokijua nasi tukifahamu kila ulipopata nafasi ya kuongea nasi. Yawezekana jitihada zako za kutupa ujuzi wako ilikuwa ni ishara ya ukomo wa maisha yako hapa duniani hivyo ulihitaji usiondoke na deni la kutompatia yeyote aliyetamani kuonja ujuzi wako wa kitaalamu.
Nyuma yako ni mbele yetu hakika
tunaomba mwenyezi Mungu akupumzishe salama.
Naamini siku moja tutakutana huko pia kwa
namna tofauti maana sote ni wapitaji hapa duniani.
Kile ulichotupatia nasi tutakitumia kuisaidia
jamii kama ishara ya kuenzi urithi uliotuachia
vichwani mwetu.
Tunawaombea wote waliopatwa na msiba huu, haswa familia yake pamoja na ndugu na jamaa Mungu awatie uvumilivu na moyo wa ujasiri katika kipindi hiki kigumu.
Familia ya wana-TRSA na wahitimu wa shahada ya usimamizi na uendelezaji wa nyanda za malisho tuko pamoja nanyi katika wakati huu mgumu.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa
jina lake lihimidiwe.
Imeandaliwa na makamu mwenyekiti TRSA
Linus, Floidin John.
No comments:
Post a Comment