NJIA ZA KUDHIBITI NDOROBO
. 1. Kuondoa vichaka. Hii ni njia iliyoanza kutumika tangu enzi za ukoloni. Ilihusisha kuondoa aidha vichaka vyote au sehemu tu ya vichaka iliyoonesha kuwa kivutio ama makazi ya ndorobo. Kwa upande wa mazingira si rafiki sababu husababisha eneo kuwa wazi hivo kuwa na madhara mengi. Hivo haitumiki sana ijapokuwa inaweza kutumika kwa kuzingatia usalama wa mazingira. 2.2. Kutumia kemikali
Hii ni njia ya kutumia dawa ya kuulia wadudu ambapo inaweza kupuliziwa kutoka angani(aerial spraying) kwa kutumia vifaa maalumu ama kupuliziwa kutokea ardhini(ground spraying), kila njia ina madhara yake na faida zake na viumbe vingine pia huweza kuathirika kutokana na kemikali inayotumika kuua ndorobo.Kemikali zinazoweza kutumika ni Dieldrin (a residual organochloride), Endosulfan (Thiodan; a non-residual organochloride) na Synthetic pyrethroids.3. Sterile male release technique
Hii ni njia inayotumika kwa kuandaa madume ya ndorobo ndani ya maabara.Madume haya huondolewa uwezo wa mbegu zake kutungisha halafu huachiliwa kwenye eneo liliothiriwa na ndorobo. Ni njia ya gharama sana. Ijapokuwa kutokana na (Bonomi et al., 2011),G. fuscipes ina onekana kuwa tofauti katika njia hii. Njia hufanya ufanisi zaidi kama eneo linalokusudiwa ni dogo pia idadi ya madume yaliyo ondolewa uwezo wa kutungisha maabara yanatakiwa kuwa na idadi kubwa kuliko madume yaliyoko eneo husika.4. Kutumia mitego
Hutengenezwa kwa kutumia kitambaa cheusi na bluu. Rangi nyeusi huwavuta ndorobo na kutua kwenye rangi nyeusi hivyo kuweza kuvutwa kwenye kifaa cha kukusanyia au sehemu ilikopakwa kemikali ya kuua ndorobo. Lakini pia kemikali za kuwavutia kama acetone, mkojo wa ngombe au mbogo huweza kutumika sababu hutoa harufu ya kuwavuta. Kuzingatia, kuna mitego ya aina nyingi kulingana na aina(spishi) ya ndorobo.Hizo ni baadhi ya njia za kudhibiti ndorobo ambazo hutumika katika maeneo yaliyo athirika na ndorobo.
IMEANDALIWA NA MAKAMU M/KITI TRSA
No comments:
Post a Comment