Forum where rangeland experts, trainees and stakeholders meet to discuss and exchange social and scientific ideas for livestock production and range ecosystem sustainability.
Thursday, 2 March 2017
WAFUGAJI WASHIRIKISHWE KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA MIMEA VAMIZI KWENYE NYANDA ZA MALISHO.
Kwa sasa maeneo yetu ya machunga yanazidi kushambuliwa na mimea vamizi. Malisho yanazidi kuteketea kwa sababu ya madhara mbalimbali yanayosababishwa na mimea hii. Hata hivyo, nafikiri elimu ikitolewa kwa mfugaji anayetumia machunga haya tunaweza kupata mafanikio chanya kabisa kuhusu kupunguza kasi ya kutapakaa kwa mimea hii vamizi.
Mimea inapovamia eneo husika mfugaji atalazimika kuhama sababu ya malisho kupoteza ubora. Kwanza mfugaji anatakiwa kuelimishwa kuwa mtafiti juu ya mmea wowote ambao hajauzoea ndani ya eneo la ikolojia. Kwa vile hawa wafugaji wanayajua vizuri maeneo yao ya machunga ni rahisi sana kugundua uwepo wa mmea mpya ndani ya eneo, hivo aelimishwe namna ya kuyakabili kwa kuyaondosha kabisa kila yanapojitokeza. Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kuzuia mimea vamizi kusambaa ndani ya machunga kwa sababu itakuwa inaondolewa kila mara inapogunduliwa kujitokeza.
MAKAMU M/KITI TRSA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment